Tanzania National Business Council

Working Groups

Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara, Mhe. Balozi John William Kijazi amezindua Vikundi Kazi vya Baraza kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania. “Lengo la kuanzisha Vikundi Kazi hivi ni kufanya interactions za kitaalam zaidi. Vikundi kazi hivyo ni Kikundi kazi cha Kilimo, Kikundi kazi chaViwanda, Kikundi kazi cha Misitu, Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara na Kikundi kazi cha Utalii. Kikundi Kazi cha Utalii hakita zinduliwa kwa sasa. Kila Mjumbe ana majukumu muhimu hivyo kuwepo kwenu kumedhihirisha upendo kulitumikia taifa letu. Vikundi Kazi hivi vitakutana mala kwa mala Kisekta na mchanganyiko wake ni Wajumbe 50 toka Sekta ya Umma na Wajumbe 50 toka Sekta Binafsi. Vikundi Kazi vitakuwa na Mwenyekiti toka Sekta ya Umma na Mwenyekiti Mwenza atatoka Sekta Binafsi.”

Kikundi kazi cha Kilimo

Kikundi Kazi cha kilimo, kinahusisha  Wafugaji, Wakulima na  Wavuvi, ni Sekta inayo ajili wengi. Kikundi Kazi hiki kinatakiwa kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa nguzo kuu za Kilimo Kwanza ili baadaye yatolewe mapendekezo yautekelezaji wa haraka wa mpango wa kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili yaani ASDP II ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Raisi hivi karibuni. Kikundi Kazi bado kinajukumu la kwenda kuchambua ilikuona ni maeneo gani Serikali na Sekta Binafsi zinatakiwa kufanyia kazi zaidi.

Kikundi Kazi cha Viwanda

Serikali inaendelea kuondoa changamoto mbalimbali. Sekta za udhibiti kama TBS na TFDA sasa hivi zinafanya kazi pamoja. TBS wameanzisha kanda tano ambazo ni Kaskazini,Kusini, Nyanda za juu kusini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati ili kusogeza huduma.

Lilikuwa wazo la Sekta Binafsi katika kikao cha 10 cha Baraza la Taifa la Biashara kwamba iundwe kamati ya viwanda ya kitaifa, sasa kikundi hiki ni muafaka na kwakuwa kina wataalamu, watachambua mambo ili kwenda mbele.  Tunategemea kikundi hiki kitakuja na mapendekezo yatakayowawezesha Watanzania wote na Wawekezaji kutoka nje  kushiriki kikamilifu katika kuifikisha nchi yetu katika uchumi imara wa viwanda.

Kikundi kazi cha Misiti

Rasilimari ya misitu Imekuwa underutilized sikuza nyuma. Ni kichocheo muhimu katika kukuza ajira kukuza uchumi wa viwanda na kutunza au uhifadhi wa mazingira. Ni mategemeo yetu kwamba wajumbe wa kikundi kazi hiki wataleta mapendekezo  naushauri ili yafanyiwe kazi.

Kkundi kazi cha Mazingira ya Biashara

Kikundi kazi cha Utalii

Comments are closed.